VIKWAZO VYA KIUCHUMI DHIDI YA SYRIA:
12 Novemba 2003Matangazo
WASHINGTON: Bunge la Marekani kwa uwingi mkubwa limekubali kuwa hatua kali zaidi zichukuliwe kuiwekea Syria vikwazo.Kuambatana na mswada wa sheria hiyo,serikali ya Damascus,miongoni mwa mambo mengine itatakwa kusitisha kuwasaidia magaidi na pia iondoshe wanajeshi wake wapatao 20,000 kutoka nchi jirani Libnani.Ikiwa Syria haitotimiza masharti hayo,hatua kali ichukuliwe kuathiri uhusiano wa kiuchumi.Na huenda pia uhuru wa kutembea wa wanadiplomasia wa Kisyria nchini Marekani ukawekewa vizuizi:na misafara ya shirika la ndege la Syria ikapigwa marufuku.Inatarajiwa kuwa Rais George W.Bush atatia saini yake katika mswada huo uliokubaliwa na baadhi kubwa ya wabunge.Mvutano uliokuwepo katika uhusiano wa Marekani na Syria,umezidi kudhoofika tangu kuzuka vita vya Iraq.Lakini mbunge wa Democrats Robert Byrd ameonya kuwa sheria hiyo baadae inaweza kujakutumiwa kwa urahisi,kupata kisingizio cha kuishambulia Syria kijeshi.
