Vikwazo vyarefushwa Kongo-Kinshasa:
19 Aprili 2005Umoja wa Mataifa:
Baraza la Usalama la Umoja awa Mataifa limerefusha muda wa vikwazo vya silaha kwa vikundi vyote vya waasi vilivyoko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Baraza hilo lenye wajumbe 15 kwa kauli moja limepitisha azimio la Ufaransa linalotaka muda wa vikwazo hivyo katika mikoa ya Mashariki mwa Kongo-Kinshasa vilivyowekwa mwaka 2003 virefushwe. Azimio linataka pia watakaovunja vikwazo hivyo wachukuliwe hatua kali. Machafuko yanayoendelea katika maeneo ya mashariki mwa Kongo-Kinshasa yanayopakana na Burundi, Rwanda na Uganda yanazorotseha juhudi za amani baada ya vita vya miaka mitano katika nchi hiyo. Azimio linapiga marufuku kwa mtu ye yote yule asiyekuwa Mwanajeshi na Polisi kuwa na silaha. Baraza la Usalama limeonyesha wasiwasi wake kutokana na ukweli kuwa kuna Wanamgambo wengi wenye silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.