Vilabu vya Ligi ya Soka Ufaransa kugoma
25 Oktoba 2013Mgomo huo wa kwanza katika soka la Ufaransa tangu mwaka wa 1972 unatarajiwa kuandaliwa katika wikendi ya mwisho ya Novemba baada ya vilabu vya nchini humo kupiga kura kwa kauli moja dhidi ya mpango huo wenye utata wa Rais Msoshalisti wa Ufaransa Francois Hollande wa kutoza kiwango kikubwa cha kodi.
Rais wa chama cha vilabu vya soka vya Ufaransa – UCPF Jean-Pierre Louvel amesema hakutakuwa na mechi mnamo tarehe 29 Novemba na Desemba 2. Chini ya mapendekezo hayo, makampuni badala ya wachezaji yatahitajika kulipa kiwango cha juu cha kodi kwa niaba ya wafanyakazi waoambao ni wachezaji ambacho kinazidi euro milioni moja.
Louvel anasema vilabu ambavyo vina wasiwasi kuwa uwezo wao wa kuwavutia wachezaji mahiri wanaopata mishahara minono kutoka ng'ambo kucheza nchini Ufaransa utakwama, vitafungua milango yao kwa mashabiki kufafanua kwa wafuasi wao ni kwanini wanahitaji kuchukua hatua hizo kali.
Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu