1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vinara Dortmund kuumana na Nuremberg

18 Februari 2019

Macho yote yatamulika Jumatatu usiku katika uwanja wa Signal Iduna Park kuona kama Borussia Dortmund watatuma ujumbe kwa mabingwa watetezi Bayern Munich

UEFA Champions League Achtelfinale | Tottenham Hotspur vs. Borussia Dortmund | Jadon Sancho
Picha: Getty Images/AFP/G. Kirk

Lakini kabla ya hayo, mwishoni mwa wiki na hasa kuhusu farasi mwingine aliyeonekana kuwa kwenye mbio za ubingwa wa ligi. Borussia Moenchengladbah walionekana kuchanganyikiwa kabisa katika jitihada zao za kutaka kupenya katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa ligi, baada ya hapo jana kukamatwa kwa sare ya 1 – 1 na Eintracht Frankfurt.

Sare hiyo ina maana kuwa Galdbach inabakia katika nafasi ya tatu na pointi 43, tano nyuma ya mabingwa Bayern Munich na saba dhidi ya vinara Borussia Dortmund. Frankfurt walikosa nafasi ya kupanda hadi nafasi ya tano na sasa wanashikilia ya saba kwenye jedwali.

Bayern walitoka nyuma na kuwalaza AugsburgPicha: Reuters/A. Gebert

Katika mechi nyingine ya Jumapili, kocha mpya Peter Bosz aliendeleza kazi nzuri katika timu ya Bayer Leverkusen kwa kupata ushindi wa 2 -0 dhidi ya Fortuna Duesseldorf dimbani BayArena na hivyo kutinga hadi nafasi ya tano. Mabao ya Leverkusen yalitumbukizwa kambani na wachezaji nyota Kai Havertz aliyefunga bao lake la tisa msimu huu, na Mjamaica Leon Bailey.

Jumamosi, Wolfsburg ilikwea hadi nafasi ya sita kwenye ligi baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Mainz, wakati Schalke na Freigburg zikitoka sare tasa matokeo ambayo yaliendelea kuziweka katika upande wa mkia wa ligi. Hoffenheim ambayo inalenga kucheza kandanda la Ulaya ilipata ushindi wa 3 – 0 dhidi ya Hanover, mechi ambayo tuliirusha live kutoka Rhein Necker Arena.

Na baada ya mabingwa watetezi Bayern Munich kupata ushindi dhidi ya Augsburg Ijumaa wa 3 – 2, macho yataelekezwa leo kwa Borussia Dortmund. BVB watashuka dimbani kupambana ugenini na Nuremberg. Dortmund wanaongoza kwa pengo la pointi mbili tu, dhidi ya Bayern. Nuremberg inashikilia mkia.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters/AP
Mhariri: Gakuba, Daniel

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW