1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vingozi wa nchi zinazoendelea wataka mifumo mipya ya fedha na uchumi Duniani.

Eva Klaue-Machangu15 Julai 2009

Zaidi ya Viongozi wa Mataifa 50 ya kutoka nchi zinazoendelea Duniani kote leo wamekutana katika mji wa Kitalii wa Sharm el-Sheikh, nchini Misr.

Naibu Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Cuba Abillardo Moreno akigonga kngele kuashuria ufunguzi wa mkutano wa NAM mjini Sharm el-Sheikh.Picha: picture alliance / Photoshot

Zaidi ya Viongozi wa Mataifa 50 ya kutoka nchi zinazoendelea Duniani kote leo wamekutana katika mji wa Kitalii wa Sharm el-Sheikh, nchini Misr, kujadili namna ya kukabiliana na tatizo la kuporomoka uchumi Duniani.


Mkutano huu wa siku mbili wa nchi zisizofungamana na upande wowote umefunguliwa na Rais wa Cuba, Raul Castro.


Katika hotuba yake ya ufunguzi Kiongozi huyo ametoa wito wa utekelezaji wa mipango mipya ya kustawisha uchumi ili kukabiliana na tatizo hilo.


Rais Castro amesema ni ukweli uliyokwisha anza kujidhihirisha kwamba mgogoro wa kiuchumi umeathiri kwa kiasi kikubwa nchi zinazoenendelea.


Amesema kutokana na hali ilivyo, pamoja na juhudi za Kiamtaifa kila nchi lazima itafute namna ya kujinasua na balaa hilo.


Akiziambia nchi Wanachama wa NAM 118 zilizokusanyika katika katika ukumbi wa Hoteli maarufu iliyopo pembezoni mwa bahari ya Sham kiongozi huyo amesema anataka kuundwe mfumo mpya wa fedha na kiuchumi ambao utakwenda sambamba na matakwa ya nchi zinazoendelea.


Sambamba na Mkutano huu Mawaziri Wakuu Yousuf Raza Gilani wa Pakistan na Manmohan Singh wa India wanatarajiwa kukutana kwa lengo la kujadili namna ya kurejesha amani katika maeneo yao ambayo ilisababisha mapigano kwa mara tatu tofauti.


Lakini hapo jana Mawaziri wa Mambo ya Kigeni Shiv Shankar Menon wa India na Salim Bashir wa Pakistan walikutana jana kwa lengo la kuanza mjadala wa suala hilo hilo kabla ya Mawaziri wakuu wao kukutana.


Mahusiano kati ya pande hizo mbili yalivurugika zaidi mwaka jana baada ya kutokea mlipuko katika mji wa kibiashara wa Mumbai na kusababisha vifo vya watu 116.


India iliituhumu Wanamgambo wa Lashkar-e-Taiba wa Pakistan kuhusika na tukio hilo.


Waziri Mkuu Singh anamatuamini kwamba Pakistan itatoa ahadi ya kuchukua hatua dhidi ya waliyofanya vitendo hivyo baada ya mkutano wake huu wa pili kufanyika tangu kutokea kwa tukio hilo mwezi Novemba mwaka jana.


Nae Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Zimbabwe Simbarashe Mumbengegwi amesema mkutano huu wa NAM utatoa fursa pana ya mjadala wa athari za mpromoko wa uchumi kwa maiatfa yanaoyendelea ambao ulianzia katika mataifa tajiri Duniani.


Amesema pamoja na jitihada zinazofanyika lakini nchi tajiri ambazo ndiyo mzizi wa tatizo hilo hazipaswi kuachwa huru katika kunuru athari kwa nci zinazoendelea.


Nchi za India pamoja na mwenyeji wa wa mkutano huo Misri ni miongoni mwa Waanzlishi wa Kundi la nchi zisizofungamana na upande wowote-NAM,ambalo ni moja kati ya kundi kubwa nje ya Umoja wa Mataifa.


NAM iliyoanzishwa mwaka 1955 inajumuisha mataifa 118 ambazo zina jumla ya asilimia 56 ya wakazi wote Duniani.


Kundi hili la linajichukulia kutofungamana na upande wowote na hasa kwa matafia makubwa jambo ambalo lilijitokeza wakati ule wa vita Baridi kati ya iliyokuwa nchi ya Kisoviet na nchi za Magharibi.


Viongozi wa NAM kwa kawaida hukutana kila baada ya miaka mitatu ambapo mkutano huu wa leo unafanyika baada ya ule uliyofanyika Quba.


Mkutano huu wa siku mbili unaambatana na maudhui yanayosema"Mshikamano wa Kimataifa kwa ajili ya amani na Maendeleo"


Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Ahmed Abdul Gheit amesema kauli mbiu hiyo ina lengo la kuleta usawa kwa wote kwa maslahi ya raia wa nchi wanachama.


Aidha Waziri huyo wa masula ya Kigeni amesema hakuna nchi itakayotengwa kwa ukubwa,nguvu za kijeshi wala uwezo wake kiuchumi.


Mwandishi-Sudi Mnette AFP/RTRE

Mhariri-Othman Miraji