1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi kushiriki kusainiwa mpango wa amani, Misri

13 Oktoba 2025

Rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ni miongoni mwa viongozi 19 watakaoshiriki hafla hiyo katika mji wa Sharm-El Sheikh nchini Misri

Viongozi wanaohudhuria hafla ya kusaini makubaliano ya kusitishwa vita Gaza, nchini Misri
Viongozi wanaohudhuria hafla ya kusaini makubaliano ya kusitishwa vita Gaza, nchini MisriPicha: Suzanne Plunkett/REUTERS

Viongozi wakuu 19 wa nchi na serikali watahudhuria baadae leo mkutano wa hafla ya kusainiwa makubaliano ya amani ya kumaliza vita Gaza, katika mji wa kitalii wa Sharm El Sheikh nchini Misri.

Rais wa Marekani Donald Trump Emmanuel Macron na Waziri mkuu Keir Starmer wa Uingereza pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  na rais wa baraza la Ulaya Antonio Costa ni miongoni mwa watakaohudhuria.

Kansela wa Ujerumani  Friedrich Merz ambaye amesema nchi yake itasimamia utekelezaji wa mpango huo wa amani unaoungwa mkono na Marekani, ameelekea Misri kushiriki hafla hiyo ambayo pia itahudhuriwa na rais wa Mamlaka ya Wapalestina  Mahmoud Abbas.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW