Viongozi wa mataifa 150 wakutana mjini Paris
30 Novemba 2015Zaidi ya viongozi hao wanakutana wa ajili ya mazungumzio ya mpango wa kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaofanyawa na binaadamu na kuepusha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabia nchi.
Washiriki wanatarajiwa kufikia makubaliano ifikapo Desemba 11, baada ya jitihada za msukumo wa awali wa viongozi wa dunia kutoonesha mafanikio ya kutosha. Miongoni mwa vikwazo vilivyotatiza maafikiano ya awali ni pamoja na nafasi ya mataifa mawili makubwa yenye kuelezwa kufanya uchafuzi mkubwa wa mazingira China na Marekani kufanya jitihada ndogo katika utekelezaji wa jitihada za ustawi wa mazingira.
Jitihada za rais Obama
Rais Barack Obama ameonesha nia ya kufikia makubalino pamoja na bunge la taifa lake kukaidi, na China imeahidi kudhibiti uzalishaji wa hewa chafu kwa kiwango kikubwa ifikapo 2030. Lakini ugumu upo katika masuala yaliyoridhiwa katika mkataba wa Kyoto 1997, likiwemo la mataifa ambayo hayakuwa yakizalisha kiwango kikubwa cha hewa chafu katika miaka ya nyuma na kwamba yapo katika mkondo wa kuelekea kuwa wazalishaji wakubwa wa hewa hizo.
Suala la siasa za ndani za Marekani linaweza kuwa tatizo lingine, pamoja na jitihada za serikali ya Obama.
Lakini kimsingi mkutano huu wanauita "mkutano wa mataifa mawili yenye kuchafua zaidi mazingira duniani", Kwa vile Obama na Xi Jinping wa China wanaketi katika mkutano mmoja na kuainisha matakwa ya mataifa yao na kuja na makubaliano ya madhubiti ya pamoja kukabiliana na mabadiliko ya taia nchi.
China inafanya uchafuzi wa mazingira kwa kutoa asilimia 30 ya hewa chafu duniani na Marekani asilimia 16. Martin Kaiser ni kiongozi wa asasi ya kimatiafa inayophusika na sera za mazingira.
Mpango wa fedha za uokozi
Katika mkutano huu wa kilele ulioanza leo, vilevile kutakauwa na lengo la kutafuta fedha za kusaidia mataifa ambayo tayari yameanza kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi, kwa kuongezeka kwa kina cha bahari na kuwepo kwa ukame wa mara kwa mara, ikijumuisha programu zenye lengo la kuchachua teknolojia mbadala na kuongeza ari ya maendeleo endelevu.
Kiasi yamataifa makubwa 20 yanatarajiwa kutangaza jitihada za kuongeza bajeti yake ya kufanywa utafiti maradufu katika nishati mbadala. Bilionea mkubwa mfanyabiashara katika tasnia ya teknolojia wa Marekani Bill Gates amekwishaonesha azma ya kuunga mkono kazi hiyo ya tafiti.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais Francois Hollande, pia watazindua muungano wa pamoja wa kimataifa katika kutangaza matumizi ya nishati ya jua ulimwenguni.
Mwandishi: Sudi Mnette DPA/APE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman