1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaDenmark

Viongozi walaani shambulio dhidi ya Waziri Mkuu wa Denmark

Sylvia Mwehozi
8 Juni 2024

Viongozi mbalimbali wa Ulaya, wamelaani vikali shambulio dhidi ya Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen
Waziri Mkuu wa Denmark Mette FrederiksenPicha: Jeremias Gonzalez/AP/picture alliance

Mwanasiasa huyo alishambuliwa katika viwanja vya mjini Copenhagen jana Ijumaa, na kuzidisha wasiwasi wa ongezeko la ghasia barani Ulaya.

Waziri Mkuu Frederiksen, mwenye umri wa miaka 46, alishambuliwa Ijumaa jioni kwa kupigwa katika viwanja vya Kultorvet na ameeleza kushutushwa na tukio hilo. Ofisi yake hata hivyo haikutoa maelezo zaidi ikiwa kiongozi huyo alijeruhiwa.

Soma pia:Waziri Mkuu wa Denmark asshambuliwa na mtu mmoja mjini Copenhagen

Mashuhuda waliozungumza na vyombo vya habari vya Denmark, wameeleza kuwa waziri huyo mkuu aliweza kuondoka kwa kutembea kutoka eneo la tukio.

Polisi tayari wanamshikilia mwanaume mwenye umri wa miaka 39 anayeshukiwa kuhusika na shambulio hilo, na amefikishwa katika mahakama mjini Copenhagen leo Jumamosi.