1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Afrika wazungumza UNGA

Admin.WagnerD26 Septemba 2018

Hotuba za viongozi wa dunia katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zimeingia siku yake ya pili mjini New York, ambako marais wa Afrika tayari wameshahutubia kikao hicho cha kila mwaka cha Umoja wa Mataifa.

USA New York Vereinte Nationen Joseph Kabila
Picha: picture-alliance/Xinhua/Q. Lang

Rais wa Kongo Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye alizungumza hapo jana alilihakikishia baraza hilo kuwa uchaguzi utafanyika nchini mwake mwaka huu, huku Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, akielezea umuhimu wa Waafrika kutatua mizozo ya Afrika wenyewe.

Rais Kabila amezikosoa vikali nchi zinazoingilia kati masuala ya ndani ya Kongo na kusema ni kinyume na misingi ya kimataifa. Huku akihakikisha kwamba taratibu ya uchaguzi nchini mwake haziwezi tena kupotoshwa. "Nimehakikisha kwamba uchaguzi uliotarajiwa Desemba mwaka huu utafanyika."

Kuingiliwa masuala ya ndani ya nchi

Rais Paul Kagame wa RwandaPicha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Rais huyo wa DRC aliendelea kusema "Hatuwezi kujenga Umoja wa Mataifa ikiwa kutakuwepo na moja wapo ya serikali inayoingilia kati maswala ya ndani ya nchi zingine. Ni mshangao kuona Umoja wa Mataifa umeendelea kuachia hali hiyo ikiendelea na kujipumbaza. Na ndio sababu msimamo wa nchi yangu ni ule wakukataa uingiliaji kati wa maswala ya ndani ya Kongo." alisema rais Kabila

Kwenye hotuba yake Rais Kabila aliomba kuondolewa  kwa wanajeshi wa Umoja Mataifa amabao amesema kazi yao haijawaridhisha Wakongomani. Miaka 20 baada ya kuletwa Kongo kikosi hicho kinaonyesha udhaifu na mafanikio yake kuhusu operesheni za kijeshi. Na kusema serikali yake imeelezea kwa mara nyingine tena lazima ya kuondolewa kwa wanajeshi hao.

Wakati Congo ikilaumiwa  na mas ya kutetea haki za binadamu,lakini rais Kabila amesema kwamba deokrasia ya nchi yake ni mfano wa kuigwa.

Kwenye sekta ya kiusalama rais kabila amelani ashambulizi ya mara kwa mara ya makundi ya wapiganaji aliyoyaita kuwa mashambulizi ya kigaidi,mfano wa huko Beni alisema.

Kwa upande wake rais wa Rwanda Paul kagame ambae alikuwa rais wa mwanzo wa Afrika kuhutubia alitioa wito wa kujenga amani na usalama barani Afrika. Huku akilezea kwamba matatizo ya Afrika lazima yatatuliwe na Waafrika wenyewe. Ameyatolea mfano makundi ya kigaidi huko Afrika Magharibi na eneo la Sahel.

Marais wengine akiwemo Cyril Ramaphosa ametoa wito wa kufanyika mageuzi katika Umoja wa Mataifa huku akiomba viti viwili vya kudumu kwenye Baraza la Usaama la Umoja wa Mataifa mahususi kwa Bara la Afrika. Mikutano mingine kadhaa  kuhusu maendeleo na kupambana na rushwa barani afrika imetarajiwa sambaba na kikao hiki cha umoja wa mataifa.

Saleh Mwanamilongo, DW New York

Mhariri: Sudi Mnette