1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

Viongozi wa Armenia na Azerbaijan kukutana Oktoba 5

24 Septemba 2023

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev watakutana katika mkutano uliopangwa kufanyika Oktoba 5 nchini Uhispania

Waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan akihutubia wanahabari mnamo Julai 25, 2023
Waziri mkuu wa Armenia Nikol PashinyanPicha: Alexander Patrin/TASS/dpa/picture alliance/dpa

Mazungumzo hayo huko Grenada yatajumuisha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel.

Waarmenia 120,000 wataondoka Nagorno-Karabakh

Taarifa hiyo inajiri wakati utawala wa jamii ya Waarmenia imesema siku ya Jumapili kuwa watu wapatao 120,000 wa huko Nagorno-Karabakh wataondoka kwenda nchini Armenia kwa kuwa hawataki kuishi katika sehemu ya Azerbaijan na kwamba wanahofia pia mauaji ya kikabila.

Rais wa Azerbaijan Ilham AliyevPicha: Press Service of the President of Azerbaijan Ilham Alijew/REUTERS

Soma pia:Waasi wa Nagorno-Karabakh kuweka chini mtutu wa bunduki

Waziri wa Mambo ya Nje wa Azerbaijan, Jeyhun Bayramov, amesema Azerbaijan, ambayo raia wengi ni Waislamu, itawaheshimu Waarmenia ambao ni Wakristo na kuwajumuisha kama raia wenye haki sawa huko Nagorno Karabakh.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW