Viongozi wa Asia-Pacifik kuzuia uchafuzi wa hewa
9 Septemba 2007Matangazo
SYDNEY.
Waziri mkuu wa Australia John Howard,akiwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa viongozi 21 wa nchi zinazopakana na bahari ya Pacifik ,amearifu kwamba viongozi hao wameafikiana kuimarisha muungano wao wa kiuchumi na kusaka njia zaidi za kukuza eneo la biashara huru la nchi za Asia-Pacifik.
Viongozi hao walikubaliana pia juu ya hatua kadhaa za kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Akieleza waziri mkuu wa Australia alisema:
„Ni hatua muhimu mno kuelekea makubaliano yenye maana sana
ya kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayotambua haja ya kupiga hatua za maendeleo na za uchumi wa aina mbali mbali unaotoa matumaini tofauti.“
Viongozi hao wa Asia-Pacifik walitoa pia mwito wa dharura kufikiwe maendeleo katika duru ya mazungumzo ya Doha kuhusu kurahisisha biashara ulimwenguni kati ya nchi tajiri na masikini kwenye sekta ya kilimo na viwanda