1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Baraza la Haki la Ulaya waungana dhidi ya Urusi

16 Mei 2023

Viongozi wa mataifa 46 yanayounda Baraza la Haki na Demokrasia barani Ulaya (CoE) wanakusanyika Iceland kuonyesha mshikamano dhidi ya Moscow.

EU-Gipfel
Picha: Nicolas Economou/NurPhoto/picture alliance

Mkutano huo unajiri mwaka mmoja baada ya Urusi kuondolewa katika Baraza hilo lenye dhima ya kutetea haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria barani Ulaya.    

Kuimarisha hatua za kuiwajibisha Urusi kisheria kwa vifo na uharibifu ambavyo imesababisha nchini Ukraine, ndizo mada zitakazogubika mkutano huo wa kilele huko Reykjavik, ambao ni mkutano wa nne pekee kufanyika katika historia ya miongo saba ya baraza hilo.

Zelenskiy aishukuru Ujerumani, Ufaransa na Uingereza

Hadi kufikia jana jioni, hakukuwa na taarifa rasmi iwapo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atashiriki katika mkutano huo.

Zelensky amefanya ziara katika miji mikuu kadhaa ya Ulaya, huku Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zikiahidi kuongeza msaada wa silaha kwa Kyiv ambayo katika wiki zijazo inatarajia kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Urusi mashariki mwa Ukraine.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW