1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Chama cha Kijani Ujerumani waamua kuachia ngazi

25 Septemba 2024

Viongozi wa Chama cha Kijani kilichomo kwenye serikali ya muungano nchini Ujerumani, wametangaza kwamba watajiuzulu nyaadhifa zao kwenye chama hicho.

Ujerumani| Chama cha kijani |Lang na Nouripour
Viongozi wa chama cha kijani cha Ujerumani Ricarda Lang na Omid NouripourPicha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance

Viongozi wa Chama cha Kijani kilichomo kwenye serikali ya muungano nchini Ujerumani, wametangaza kwamba watajiuzulu nyaadhifa zao kwenye chama hicho.

 Viongozi hao Ricarda Lang na Omid Nouripour, wametangaza hii leo Jumatano kuwa watendaji wa chama cha Kijani cha walinda mazingira watajiuzulu ifikapo mwezi Novemba baada ya chama hicho kushindwa vibaya kwenye chaguzi kadhaa za mikoa.

Katika ngazi ya kitaifa, chama hicho cha Kijani ni cha pili kwa ukubwa katika serikali ya muungano ya vyama vitatu inayoongozwa na Kansela Olaf Scholz, wa chama cha SPD.

Miongoni mwa matukio mabaya ya hivi karibuni kwa chama hicho cha Kijani ni uchaguzi uliomalizika wa siku ya Jumapili katika jimbo la mashariki mwa Ujerumani la Brandenburg, ambapo chama hicho kilipoteza viti vyote katika bunge kwenye jimbo hilo baada ya kushindwa kufikia kiwango cha asilimia 5 kinachohitajika ili kupata uwakilishi bungeni katika uchaguzi wa Ujerumani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW