1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchango wa ufadhili wa utafiti wa chanjo ya Corona waanza

4 Mei 2020

Muungano wa viongozi wa dunia baadaye utafanya mkutano wa kilele unaotarajiwa kuchangisha mabilioni ya dola kufadhili shughuli za utafiti wa chanjo ya kukabiliana na virusi vya Corona

Kanada Coronavirus Notaufnahme des Vancouver General Hospital in Vancouver
Picha: picture-alliance/empics/The Canadian Press/J. Hayward

Fedha hizo pia zitasaidia katika utafiti wa utengenezaji wa tiba mpya na upimaji wenye uhakika zaidi. Kwa mujibu wa chuo kikuu cha Johns Hopkins takriban watu milioni 3.5 wameambukizwa virusi hivyo duniani na zaidi ya 247,000 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

Mkutano huo utakaofanyika kwa njia ya video unalenga kukusanya dola bilioni 4.37 kwa ajili ya kusaidia katika utafiti wa chanjo, takriban  bilioni 2 kwa ajili ya tiba na dola bilioni 1.64 kwa ajili ya shughuli za upimaji.

Maafisa wanasema kiwango hicho cha fedha ni cha mwanzo tu kwa sababu fedha zaidi zitahitajika katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo kwa ajili ya utengenezaji na usambazaji wa chanjo na tiba.

Kwenye taarifa iliyotolewa kabla ya mkutano huo, viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, Italia, Norway na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya wamesema fedha zitakazochangishwa zitatolewa zaidi kwa mashirika ya afya yanayotambuliwa duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW