1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Viongozi wa dunia wakusanyika Paris kwa ajili ya Notre-Dame

7 Desemba 2024

Viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo rais mteule wa Marekani Donald Trump leo wanahudhuria kufunguliwa rasmi tena kwa Kanisa Kuu la Notre-Dame mjini Paris.

Notre-dame
Kanisa la Notre-dame mjini ParisPicha: Thibault Camus/AP Photo/picture alliance

Viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo rais mteule wa Marekani Donald Trump leo wanahudhuria kufunguliwa rasmi tena kwa Kanisa Kuu la Notre-Dame mjini Paris.

Taarifa za ndani zinasema Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewaalika viongozi 50 wa dunia katika ufunguzi wa kanisa hilo ambalo lipo katikati mwa mji mkuu wa Ufaransa wa Paris na ambalo lilichomwa moto wakati wa moto mkubwa mwaka 2019.

Soma zaidi: Macron aapa kusalia madarakani baada ya serikali kuporomoka

Viongozi wengine watakaohudhuria tukio hilo ni pamoja na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Italia Sergio Mattarella.

Trump alitangaza kuhudhuria tukio hilo siku chache zilizopita kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social na hii itakuwa ni safari yake ya kwanza nje ya Marekani tangu ushindi wake wa uchaguzi mapema mwezi Novemba.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW