1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa dunia wampongeza Donald Trump

Angela Mdungu
6 Novemba 2024

Viongozi mbalimbali wa dunia wamejitokeza kumpongeza Donald Trump kwa ushindi wake dhidi ya mgombea wa Democratic ambaye pia ni makamu wa Rais, Kamala Harris.

Israel, Tel Aviv | Bngo la kumpongeza Trump
Bango la pongezi rais mteule wa Marekani Donald Trump likiwa katikati mwa mji wa Tel AvivPicha: Thomas Peter/REUTERS

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kupitia ukurasa wake wa X amempongeza Trump kwa ushindi wake aliouita wa kihistoria. Amesema kurejea kwake katika ikulu ya White House ni mwanzo mpya kwa Marekani na kwa ushirikiano mkubwa kati ya Israel na Marekani.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema ataendelea kushirikiana na Marekani kwa manufaa ya raia wa nchi hizo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Stammer amesema ana matumaini ya kufanya kazi na Trump katika miaka ijayo. Ameongeza kuwa kama washirika wa karibu nchi yake na Marekani zinasimama bega kwa bega katika kulinda maadili ya pamoja ya  uhuru, demokrasia na biashara.

Soma zaidi: Trump ajitangaza mshindi wa urais Marekani

Kwa upande wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amempongeza Trump na kuweka wazi kuwa yuko tayari kufanya kazi pamoja kama ilivyokuwa katika miaka minne ya utawala wake.

Je Kamala anaweza kumshinda Trump katika uchaguzi 2024?

01:58

This browser does not support the video element.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte ametoa pia pongezi kwa Trump kwa kushinda uchaguzi huo. Amesena uongozi wa Trump utakuwa muhimu katika kuiimarisha Jumuiya hiyo.

Baada ya Trump kujitangaza mshindi mapema Jumatano, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel amesema Umoja wa Ulaya na Marekani zina ushirikiano wa muda mrefu na uhusiano wa karibu wa kihistoria.

Naye Rais wa Halmashauri ya umoja huo Ursula Von der Leyen ameeleza kuwa anatazamia kufanya kazi pamoja na Trump kwa mara nyingine ili kuendeleza ajenda muhimu ya kimataifa.

Soma zaidi:Uchaguzi wa Marekani: Nini kinatokea siku ya uchaguzi na baadae?

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kuwa nchi yake inaendelea kutegemea ushirikiano wa Marekani na amempongeza Trump kwa ushindi wake mkubwa. 

Kwa upande, ikulu ya Kremlin imesema Rais Vladmir Putin hana mpango wa kumpongeza Trump, huku ikiongeza pia kuwa Moscow haijaingilia uchaguzi wa Marekani.

Naye Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ameutaja ushindi wa Trump kuwa mkubwa zaidi katika historia ya siasa za Marekani na kuwa unahitajika sana duniani.

Wengine waliotoa pongezi kwa Donald Trump ni pamoja na Waziri Mkuu wa India Narendra Mordi, Georgia Meloni wa Italia, Naibu wake Matteo Salvini, Kansela wa Austria Karl Nehammer na Geert Wilders wa Uholanzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW