1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECOWAS yasema inakabiliwa na ukosefu wa usalama wa kikanda

23 Juni 2025

Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo na Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wamekiri kwamba kanda hiyo iko matatani, ikikabiliwa na ongezeko la machafuko na ukosefu wa utulivu wa kisiasa.

ECOWAS , CEDEAO, AES, Mali, Niger, Burkina Faso, Gipfel, Nigeria , Politik
Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo na Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi - ECOWAS yakiri kanda hiyo inakabiliwa na ongezeko la machafuko.Picha: Ubale Musa/DW

Rais Julius Maada Bio wa  Sierra Leone, aliyechukua uwenyekiti wa kupokezana wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Rais Bola Tinubu wa Nigeria, alisema Afrika Magharibi inapitia changamoto kubwa.

Niger, Burkina Faso na Mali zaombwa kurejea ECOWAS

Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa usalama katika kanda ya Sahel na mataifa ya pwani, ugaidi, ukosefu wa utulivu wa kisiasa, upitishaji wa silaha kimagendo na uhalifu wa kupangwa. 

Katika mkutano wa viongozi hao uliofanyika jana mjini Abuja, Nigeria, Maada Bio alisema muda umefika wa kushirikiana kikamilifu kiusalama, ikiwemo kuwa na kitengo cha pamoja cha ujasusi na kitengo cha utoaji wa majibu ya haraka. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW