1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa EU kujadili mustakabali wa utawala mpya Syria

19 Desemba 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo hii kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa zamani wa Syria, Bashar al-Assad.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya
Mataifa ya umoja wa Ulaya yanakabiliwa na maamuzi ya namna gani ya kushughulika na uongozi mpya wa taifa hiloPicha: Alexandros Michailidise/European Union

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa zamani wa Syria, Bashar al-Assad, wakati ambapo mataifa ya umoja huo yanakabiliwa na maamuzi ya namna gani ya kushughulika na uongozi mpya wa taifa hilo.

Soma pia: EU kuanzisha mawasiliano na utawala mpya wa Syria

Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen amesema vikwazo vya kiuchumi vya Umoja wa Ulaya kwa Syria vinaweza kuangaliwa upya iwapo uongozi mpya wa nchi hiyo utaonyesha dhamira kuelekea mabadiliko ya kidemokrasia jumuishi na kipindi cha mpito cha makabidhiano ya madaraka. 

Alexander De Croo ni Waziri Mkuu wa Ubelgiji. "Nadhani ni muhimu kwamba uhuru wa kimipaka wa eneo la Syria uheshimiwe. Kila jihudi inapaswa kufanya ili kutuliza hali hiyo ili kwa mfano, watu wanaotaka kurejea nyumbani waweze kurudi. Tunapaswa kuwa na tahadhari kwamba Syria ni mahali ambapo mzozo wa kikanda unaohusisha nchi nyingi unaweza kutokea. Kwa hivyo takwa letu ni kusimamisha vurugu na tuheshimu uhuru mipaka ya  Syria."

Kundi linaloongoza serikali mpya ya Syria  la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), ambalo kwa sehemu kubwa ni limehusika katika kupinduliwa kwa al-Assad,  limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na pia linakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW