1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa EU wakutana kujadili matokeo ya uchaguzi

17 Juni 2024

Viongozi 27 wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wapo mjini Brussels kutathmini matokeo ya uchaguzi wa bunge la Ulaya na kuanza mchakato wa kutafuta viongozi wakuu wa Umoja huo.

Wananchi wa maraifa ya Ulaya wakifuatilia matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya.
Wananchi wa maraifa ya Ulaya wakifuatilia matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Ulaya.Picha: Christoph Schmidt/dpa/picture alliance

Uchaguzi wa bunge la Ulaya uliofanyika tarehe 6 hadi 9 mwezi huu wa sita ulivipa mafanikio vyama vya siasa kali vya mrengo wa kulia na kuvishangaza vyama vya siasa za wastaninchini Ujerumani na Ufaransa. Hii inamaanisha nguvu ya Ujerumani na Ufaransa inayochangia pakubwa siasa ya Ulaya kidogo imedhoofika. 

Soma pia:Ulaya inajigamba kudhibiti uingiliaji kwenye uchaguzi wake

Kulingana na sheria za umoja huo, marais na mawaziri ndio walio na nafasi ya kumchagua rais wa Halmashauri kuu ya Umoja huo atakayehudumu kwa miaka mitano hadi mwaka 2029. Halmashauri hiyo ndio inayoamua kuhusu bajeti ya miaka saba ijayo ya Umoja huo pamoja na  sera zake juu ya kila kitu ikiwemo masuala ya mazingira. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW