1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Viongozi wa EU wakutana na rais Volodymyr Zelenskiy

3 Februari 2023

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy mjini Kyiv wakiwa na ahadi ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi lakini bila ya matumaini ya kuikaribisha haraka Ukraine ndani ya Umoja wa Ulaya.

Von der Leyen mit EU-Kommission zu Gesprächen in Kiew
Picha: Uncredited/Ukrainian Presidential Press Office/AP/dpa/picture alliance

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen yuko mjini Kyiv tangu jana alikowasili kwa treni, katika safari iliyonuiwa kuwa ishara ya kuonesha uungaji mkono kwa taifa hilo linaloelekea kuadhimisha mwaka mmoja tangu uvamizi wa Urusi.

Hii leo Bibi von der Leyen na rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya Charles Michel watakuwa na mkutano na rais Zelenksy utakaofanyika baada ya mazungumzo ya maafisa waandamizi kutoka pande zote mbili.

Rais Zelensky ameurai Umoja wa Ulaya kuongeza vikwazo dhidi ya Moscow lakini duru zimedokeza kwamba awamu mpya ya vikwazo vinavyoandaliwa na umoja huo haitokidhi matakwa ya serikali mjini Kyiv.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW