1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G20 watofautiana kuhusu maadili

28 Juni 2019

Viongozi wa mataifa ya G20 wanaokutana Japan wanatofautiana juu ya maadili yaliohudumu kwa miongo kadhaa kama msingi wa ushirikiano wao, huku wakikabiliwa na miito ya kuepusha vitisho kwa ukuaji wa uchumi wa dunia.

Vor dem G20-Gipfel in Osaka
Picha: picture alliance/dpa/J. C. Hong

Akifungua mkutano huo wa siku mbili mjini Osaka jana Ijumaa, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe aliainisha umuhimu wa biashara huru, akisema inaweka msingi wa amani na maendeleo, na kuonya pia dhidi ya sera za ulinzi wa biashara za ndani alizosema zina manudaa kidogo sana.

"Mabadiliko makubwa yaliosababishwa na utandawazi huenda yakazusha wasiwasi na kutoridhika na pia makabiliano makali baina ya mataifa. Mifuno ya ulinzi wa kibiashaea ya kulipizana haitalinufaisha taifa lolote.

Hatua zozote za kibiashara zinahitaji kuwiana na makubaliano ya shirika la biashara duniani WTO. Nina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya sasa ya uchumi wa dunia.

Dunia inafuatilia mwelekeo tutakaouchukuwa sisi, viongozi wa G20. Tunahitaji kutuma ujumbe mzito, ambao ni kuunga mkono mfumo wa biashara ulio huru, wa haki na usiobagua," alisema Abe.

Mgawanyiko miongoni mwa viongozi

Wakati makundi kama G20 yanajaribu kujenga muafaka kuhusu mikakati mipana ya kisera na masuala ya siasa za kikanda,  pia yamegawanyika kuhusu masuala kadhaa.

Akipuuza onyo la China kutogusia maandamno ya karibuni mjini Hong Kong, Abe alimuambia rais wa China Xi Jinping kwamba ilikuwa muhimu kwa Hong Kong huru na iliyo wazi kustawi chini sera ya nchi moja, mifumo miwili, walisema maafisa wa Japan, wakimaanisha utaratibu wa koloni hilo la zamani la Uingereza, lilipokabishiwa kwa China mwaka 1997.

Waziri Mkuu Shinzo Abe (kushoto) akisalimia na Rais wa China Xi Jinping kabla ya kunaza kwa mkutano wa G20 mjini Osaka, Juni 27,2019.Picha: picture-alliance/AP Images/The Yomiuri Shimbun

Walisema Abe alimkubusha Xi juu ya umuhimu wa kuhakikisha uhuru, haki za binadamu, utawala wa sheria na maadili mengine ya kimataifa katika kuelezea wasiwasi kuhusu sheria ya Hong Kong ambayo ikiwa itapitishwa, itaruhusu kuepelekwa watuhumiwa kushtakiwa China bara.

Sheria hiyo iliyowekwa kapuni kwa sasa, ilisababisha maanmano makubwa ya wakaazi wa Hong Kong na mengine madogo katika maeneo mengine barani Asia, ikiwemo katika mji wa Osaka.

Siyo Xi pekee anaekosolewa

Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk alishambulia rais wa Urusi Vladmir Putin kwa kusema katika mahojiano na gazeti la Financial Times, kwamba uliberali umepitwa na wakati na unakinzana na idadi ya waliowengi zaidi katika mataifa mengi.

Tusk aliwambia waandishi habari kwamba wao kama Waulaya wanatetea kwa nguvu zote na kutanga demokrasia ya kiliberali, na kwamba anachokiona kimepitwa na wakati ni utawala wa kiimla, umaarufu wa mtu mmoja, na utawala wa kikundi cha wachache, hata kama wakati mwingine wanaweza kuoneka wenye ufanisi.

Tusk alisema matamshi kama yanaleta fikra ya imani kwamba uhuru umepitwa na wakati, kwamba utawala wa sheria umepitwa na wakati na kwamba haki za binadamu zimepitwa na wakati.

Putin alimsifu rais Donald Trump kwa juhudi zake za kujaribu kuzuwia wimbi la wahamiaji na madawa kutoka Mexico, na kusema kwamba uliberali unadhani kwamba hakuna kinachotakiwa kufanyika.

Kwamba wahamiaji wanaweza kuua, kuharibu na kubaka bila kushtakiwa kwa sababu haki zao kama wahamiaji zinapaswa kulindwa.

Viongozi wakuu wa mataifa yanaounda kundi la G20 wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa kilele wa kundi hilo, Osaka, Japan, Juni 28, 2019.Picha: President Secretary/Laily Rachev

Muafaka kati ya Xi, Modi na Putin

Trump amejikuta mara nyingi katika mkwaruzano na viongozi wengine katika matukio ya kimataifa kama hilo, hasa kuhusiana na masuala kama vile Iran, mabadiliko yatabianchi na biashara.

Kwenye mkutano kandoni mwa G20, Putin, Xi na waziri mkuu wa India Narendra Modi walikubaliana juu ya haja ya kuamini sheria ya kimataifa, kuheshimu uhuru wa kitaifa na kujizuwia kuingia masuala ya ndani ya mataifa mengine, alisema Putin.

Matamshi kama hayo ni vijembe kwa sera ya Trump ya Amarika Kwanza katika kukataa ushirikiano wa mataifa mengi, lakini pia yanachora msitari dhidi ya ukosoaji wa serikali za kiimla kama za China na Urusi.

Mkutano wa kihistoria

Abe anataka kuufanya mkutano wa kilele wa Osaka kuwa wa kihistoria kwa ajili ya maendeleo kuhusu masuala ya mazingira, ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, kuhusu ushirikiano katika kutunga sheria mpya za uchumi wa kidijitali, na kuimarisha tahadhari dhidi ya matumizi mabaya ya teknolojia kama vile sarafu za mtandaoni kufadhili ugaidi na uhalifu mwingine unaohusiana na intaneti.

Kuhusu mzozo kati ya Iran na Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alismea dunia haiwezi kumudu mgogoro huo na ni muhimu kutuliza hali, na kuepuska makabiliano.

Katika barua kwa viongozi hao mjini Osaka, Guterres alihimiza hatua kuhusu mageuzi ya usawa na imara kuimarisha usalama wa kifedha duniani na kuongeza unyumbulifu wa uchumi wa dunia.

Vyanzo:ape,aptn

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW