Viongozi wa G7 kufanya mkutano wa siku tatu nchini Canada
15 Juni 2025
Matangazo
Mbali na mvutano huo wa Mashariki ya Kati, viongozi hao pia wanatarajiwa kuangazia vita nchini Ukraine, mizozo ya biashara ya kimataifa, uhamiaji, na kupata ufikiaji wa malighafi muhimu.
Mazungumzo ya pembezoni mwa mkutano huo pia yanatarajiwa.
Mkutano wa G7 waijadili Ukraine na uchumi wa dunia
Watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer.
Waziri mkuu wa Canada Mark Carney ni mwenyeji mkutano huo, unaokuja baada ya ushindi wake katika uchaguzi, ambao kwa sehemu umetokana na msimamo wake mkali dhidi ya tishio la Trump la kuifanya Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani.