1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G7 wakubali kuzuia uagizaji wa almasi za Urusi

7 Desemba 2023

Viongozi wa kundi la mataifa tajiri ulimwenguni la G7 wamekubaliana kuzuia uingizwaji wa almasi ya Urusi kuanzia mwaka ujao, hii ikiwa ni hatua mojawapo ya kuzidhisha makali ya vikwazo dhidi ya serikali ya taifa hilo

Japan G7 Außenministertreffen
Picha: Jonathan Ernst/Pool/dpa/picture alliance

Viongozi hao wamesema kwenye taarifa yao kwamba hatua hiyo itafuatiwa na vizuizi zaidi vya hatua kwa hatua juu ya uagizaji wa almasi za Urusi zilizochakatwa. Vikwazo hivyo vipya vinaongeza msururu wa vikwazo ambavyo Urusi imewekewa na Marekani na nchi nyingine kufuatia uvamizi wake wa Februari 2022 nchini Ukraine. Vikwazo vya awali vililenga taasisi za fedha, uagizaaji wa teknolojia na mauzo ya nje ya nishati.Katika hotuba yake kwa viongozi waG7 siku ya Jumatano, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alionya dhidi ya kusambaratika kwa ushirika wa magharibi, akisema kuwa Urusi inategemea hilo kutokea mwaka ujao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW