1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mazungumzo kati ya Iran na Marekani kufanyika Roma Jumamosi

17 Aprili 2025

Viongozi wa Ghuba na Mashariki ya Kati wameanza ziara katika mataifa mbalimbali kabla ya kuanza siku ya Jumamosi mjini Roma, kwa duru ya pili ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani juu ya mpango wa nyuklia wa Tehran.

Mazungumzo kati ya Marekani na Iran kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi akizungumza na wajumbe wa nchi yake wakati wa duru ya kwanza ya mazungumzo na Marekani huko mjini Muscat, Oman.Picha: KhabarOnline/AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi na Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani wamewasili mjini Moscow ambapo wanatarajiwa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, huku Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia Mwanamfalme Khalid bin Salman akielekea mjini Tehran.

Duru ya kwanza ya  mazungumzo kati ya Marekani na Iran  ilifanyika mjini Muscat huko Oman, katika wakati ambapo rais Donald Trump na Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei wamekuwa wakirushiana maneno makali na vitisho.

Hata hivyo mazungumzo hayo yanatarajiwa kuwa magumu kwa kuwa Iran imesisitiza kwamba haki yake ya kurutubisha madini ya urani haiwezi kuwa sehemu ya majadiliano.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW