Viongozi wa Jumuiya ya SADC kujadili machafuko ya Msumbiji
15 Novemba 2024Matangazo
Siku ya Jumatano, watu wawili waliripotiwa kuuawa mjini Maputo baada ya polisi kujaribu kuyazima maandamano ya upinzani huku mpaka na Afrika Kusini ukifungwa.
Msumbiji imetumbukia katika mzozo wa kisiasa baada ya upinzani kuyapinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9 ambayo yamesababisha maandamano ya mara kwa mara.
Upinzani unasema kuwa matokeo yamechakachuliwa na kukipendelea chama tawala cha FRELIMO. Mataifa mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini yametoa wito wa kurejeshwa hali ya utulivu na utawala wa sheria nchini Msumbiji.