Viongozi wa Kenya na Haiti wakutana Nairobi
11 Oktoba 2024Matangazo
Viongozi hao wamesema ujumbe huo unahitaji rasilimali zaidi na kwamba bajeti yake itamalizika Machi mwaka 2025. Umoja wa Mataifa uliahidi kutoka dola milioni 85 kuusaidia ujumbe huo, lakini umetowa milioni 68 mpaka sasa.
Rais William Ruto, aliyekutana Nairobi na Waziri Mkuu wa Haiti, Garry Conille amesema nchi yake itapeleka askari 600 zaidi mwezi Ujao.
Kenya ambayo inaongoza ujumbe huo wa kumaliza vurugu zinazosababishwa na magenge, imepeleka takriban maafisa 400 nchini Haiti wanaoshirikiana na wanajeshi na polisi kutoka Jamaica.
Nchi zilizoahidi kuchangia wanajeshi, ikiwemo Chad, Benin, Bangladesh na Barbados zimeshindwa kuchukua hatua hiyo hadi sasa.