1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Kiarabu wana chaguo lipi katika mzozo wa Gaza?

24 Januari 2024

Hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, pamoja na hasira ya umma, vimezidisha shinikizo kwa viongozi wa mataifa ya kiarabu kuchukua hatua juu ya mzozo wa Gaza huku baadhi ya hatua kali zikipendekezwa.

Algeria, viongozi wa mataifa ya Kiarabu
Baadhi ya viongozi wa mataifa ya Kiarabu huko Algeria mwaka 2022Picha: Tunisian Presidency/REUTERS

Mapema miaka ya 70, mataifa ya Kiarabu yanayozalisha mafuta kwa wingi yalianzisha marufuku ya uuzaji mafuta kwa Marekani na mataifa mengine yakiwemo Uholanzi na Ugiriki katika hatua ya kuyaadhibu kwa kuiunga mkono Israel. Marufuku hiyo inaelezwa kuwa ndio mzozo wa kwanza wa mafuta ulimwenguni. Mnamo mwaka 1973, Syria na Misri zilifanya mashambulizi dhidi ya Israel katika jaribio la kuyadhibiti tena maeneo yaliyonyakuliwa na na Israel baada ya vita vya mwaka 1967 kati ya Israel na nchi za Kiarabu ikiwemo Rasi ya Sinai na vilima vya Golan.Mataifa ya kiarabu yahofia uhamisho mpya wa Wapalestina

Mkutano wa jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiarabu uliofanyika Misri 2023Picha: Ahmed Gomaa/Xinhua/IMAGO

Mataifa mengine ya Kiarabu kama Saudi Arabia ambayo ni mzalishaji mkuu wa mafuta iliunga mkono juhudi hizo zilizofahamika wakati huo kama "silaha ya mafuta". Marufuku hiyo ya mafuta ilidumu hadi mwaka 74 na kuwa na athari kubwa. Bei za mafuta ulimwenguni zilipanda kwa asilimia 300, mfumuko mkubwa wa bei, uhaba wa petroli na ghadhabu kali ya umma huko Marekani. Lakini marufuku hiyo pia iliwalazimu wanadiplomasia wa Marekani kuingilia kati mzozo huo kwa kuwaleta pamoja Wamisri na Waisraeli waliokuwa wakipigana kwa wakati huo katika meza ya mazungumzo.

Je Kwanini sasa kusitumike nyenzo hiyo ya "silaha ya mafuta"? Baadhi ya nchi ikiwemo Algeria na Lebanon zilipendekeza katika mkutano wa mwezi Novemba huko Saudi Arabia ambako viongozi wa mataifa ya Kiarabu walikutana kujadili wanavyoweza kuushughulikia mzozo wa Gaza. Wazo hilo lilipingwa kwa haraka sana, huku maafisa wa Saudia ambayo ni mshirika muhimu katika marufuku hiyo ikilikataa wazo hilo moja kwa moja. 

Mtizamo wa nchi za Kiarabu: Nchi za kiarabu na Ulaya zapigia debe suluhisho la mataifa mawili mzozo wa Mashariki ya Kati

Kwanini Afrika Kusini inaishtaki Israel ICJ?

02:26

This browser does not support the video element.

Khaled Elgindy ambaye ni Mkurugenzi wa programu ya masuala ya Israel na Palestina katika taasisi ya Mashariki ya Kati anasema kuwa, linapokuja suala la kuushughulikia mzozo wa Gaza, mataifa ya Kiarabu yanakabiliwa na "mkanganyiko". Ameieleza DW kwamba mataifa hayo "yanajaribu kupima uwiano tofauti wa kimaslahi, upande mmoja  yanataka kuonyesha umma wake ambao umekasirishwa na Israel na Marekani, kwamba wanawaunga mkono Wapalestina. Lakini upande mwingine hayataki kufanya jambo lolote ambalo litadhoofisha uhusiano wake na Marekani.

Mkurugenzi huyo anasema marufuku ya kimataifa ya mafuta itasababisha "makabiliano ya moja kwa moja na Marekani na mataifa mengine ya nchi za Magharibi", ndio sababu hakuna uwezekano wa nyenzo hiyo kutumika.

Soma hii: Mataifa ya kiisalam yaikosoa Marekani katika vita ya Gaza

Lakini wakati huo huo mataifa hayo ya Kiarabu yamekabiliwa na shinikizo kubwa la kuchukua hatua. Idadi ya vifo katika Ukanda wa Gaza imepanda na kufikia 25,000 kwa mujibu wa wizara ya afya kwenye ukanda huo unaoongozwa na Hamas. Umoja wa Mataifa, pia umeonya kwamba idadi ya wakaazi wa Gaza iko katika kitisho cha kukabiliwa na baa la njaa na magonjwa kwasababu ya mzingiro wa Israel. Baadhi ya wanasiasa wa mataifa ya Kiarabu ikiwemo Qatar na Jordan wameonya kitisho cha vita vya kikanda na ongezeko la itikadi kali miongoni mwa raia wake.

Kuundwa kwa taifa huru la Palestina: Mataifa kadhaa ya Mashariki ya kati yaahidi kuunga mkono juhudi za kuundwa taifa la Palestina

Waandamanaji wakishika mabango ya kutaka kukomeshwa vita Gaza huko Dubai wakati wa COP28Picha: AMR ALFIKY/REUTERS

Jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiarabu, ilitoa azimio baada ya kukutana mjini Cairo Misri siku ya Jumatatu, linalosema kwamba mataifa ya Kiarabu "yatazingatia hatua zote za kisheria, kidiplomasia na kiuchumi ili kuzuia Wapalestina kugeuka wakimbizi". Hata hivyo Bw. Elgindy anasema baadhi ya hatua hizo hazina mashiko kwasababu, nchi hizo haziwezi kupeleka silaha katika Ukingo wa Magharibi wala wapiganaji. Lakini hata hivyo anatoa mapendekezo ya nini kinachoweza kufanyika, ikiwa ni pamoja na kuwafukuza mabalozi wa Israel, kusambaza misaada ya kiutu, kuzuia usambazaji wa silaha za Marekani kupitia kambi za Washington zilizoko kwenye mataifa ya Kiarabu na vilevile kuungana na Afrika Kusini katika kesi yake dhidi ya Israel katika mahakama ya kimataifa ya haki ya ICJ.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW