Watoto zaidi ya 200,000 walinyanyaswa kingono Uhispania
27 Oktoba 2023Ripoti hiyo haikutoa takwimu halisi lakini imesema uchunguzi wa maoni wa zaidi ya watu 8,000 uligundua kuwa asilimia 0.6 ya karibu jumla ya watu wazima milioni 39 nchini Uhispania walisema walinyanyaswa kingono na makasisi wakati wakiwa watoto.
Ufichuzi huo nchini Uhispaniandio wa karibuni kulikumba Kanisa Katoliki baada ya mfululizo wa kashfa za unyanyasaji wa kingono kote ulimwenguni, aghalabu ukiwahusisha watoto, kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Soma pia:Papa Francis akemea unyanyasaji wa kingono unaofanywa na makasisi Ureno
Ripoti hiyo imekosoa mtizamo wa Kanisa Katoliki, ikitaja mwitikio wake wa kesi za unyanyasaji wa watoto unaohusisha makasisi kuwa usiotosha.
Imependekeza kuundwa kwa mfuko maalum wa serikali kuwalipa fidia waathiriwa. Jukwaa la maaskofu wa Uhispania litafanya mkutano wa dharura Jumatatu ijayo kujadili matokeo ya uchunguzi huo.