1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa kidini wazindua kampeni ya amani mashariki Kongo

14 Machi 2023

Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kikristu huko mkoani kivu ya kaskazini wamezindua mpango wa kuhimiza amani na kuyahimiza makundi ya waasi ikiwemo hilo la wapiganaji wa M23 kusitisha mapigano.

DR Kongo Proteste gegen die Gewalt im Osten
Picha: Justin Makangara/REUTERS

Vyanzo kutoka mashirika ya kiraia katika maeneo mbalimbali wilayani Masisi, vimehakikisha taarifa ya kuanza kuondoka kwa waasi hao wa M23 katika mji mdogo wa Mweso, Kiuli, Malehe na kwenye milima inayoinukia kijiji cha Karuba ambako misururu ya wapiganaji hao ulionekana wote wakiwa wamebeba mizigo na silaha lakini bila kueleza ni wapi walielekea, kama anavyoshuhudia mkaazi huyu wa kitshanga ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Soma pia: Usalama wazidi kuzorota nchini Kongo

Hata hivyo, upande wa mashirika ya kiraia  wamesema kuwa na mashaka kufuatia hatua hiyo ya M23 kwa kile wanachotaja kama ujanja wa kuendelea kuvishikilia vijiji vingine

Wakati huo huo, katika mkutano wao na vyombo vya habari ,viongozi wa madhehebu mbalimbali mkoani kivu kaskazini  walikutana hiyo jana hapa mjini ambapo walijadili hali jumla ya usalama mkoani Kivu kaskazini ambako Wakuu  hao kutoka madhehebu mbalimbali ya kidini wamewataka wananchi  kukuza amani  ambayo ni njia pekee ya kuzima mzozo unaoendelea kufukuta kati ya serikali na kundi la waasi wa M23 

Soma pia: M23 wakabiliana na jeshi na kukaidi amri ya kusitisha mapigano Kongo

Haya yanajiri siku moja  baada ya ziara ya siku 3 ya wajumbe wa baraza la umoja wa mataifa hapa nchini Congo ,waliolitaka kundi hilo la  waasi wa M23  kuondoka na kuyaacha maeneo yote linalodhibiti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW