1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Viongozi wa kijeshi wa Niger kujibu uchokozi

4 Agosti 2023

Viongozi wa mapinduzi wa Niger wamesema watajibu mara moja jaribio lolote la kichokozi dhidi ya nchi hiyo na nchi nyingine za Afrika Magharibi.

General Abdourahmane Tiani
Picha: REUTERS

Hii ikiwa ni siku tatu kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho uliotolewa na jumuiya ya kikanda ya ECOWAS wa kurejesha utulivu.

ECOWAS ilikuwa imetishia uwezekano wa kutumia nguvu ikiwa viongozi wa kijeshi hawatomrejesha Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum ifikapo siku ya Jumapili. Jumuiya hiyo pia ilitangaza vikwazo vya kibiashara na kifedha baada ya mapinduzi.

Soma pia: Mtawala wa kijeshi Niger aonya dhidi ya uingiliaji wa kigeni na kuutaka umma kuilinda nchi

Viongozi wa mapinduzi pia wametangaza kuwasimamisha mabalozi katika nchi nne, pamoja na kufuta ushirikiano wa kijeshi baina ya nchi hiyo na Ufaransa. Mabalozi wa waliovuliwa majukumu ni katika nchi za Ufaransa, Nigeria, Togo na Marekani.

Uamuzi huo umetolewa wakati uongozi wa kijeshi ukizidi kukabiliwa na shinikizo la kumrejesha madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum.