SiasaAsia
Korea Kusini na Japan zajadili kuboresha uhusiano wao
7 Mei 2023Matangazo
Viongozi wa Korea Kusini na Japan, katika muda usiozidi miezi miwili wamekutana leo kwa kikao cha pili cha mazungumzo juu ya kushughulikia mivutano ya kihistoria kati ya nchi hizo vilevile kuboresha uhusiano wao na kuzikabili changamoto zinazotokana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. Na kwa ajili hiyo waziri mkuu wa Japan, Fumio Kishida anafanya ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini baada ya mwenzake wa Korea Kusini rais Yoon Suk Yeol kufanya ziara nchini Japan mnamo mwezi Machi. Vyombo vya habari vya Korea Kusini vinasubiri kuona iwapo waziri mkuu wa Japan ataomba radhi kwa uwazi zaidi juu ya udhalimu wa ukoloni wa Japan nchini Korea Kusini kuanzia mwaka 1910 hadi mwaka 1945.