1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Kundi la G20 waanza kuwasili Afrika Kusini

21 Novemba 2025

Viongozi wa dunia wameanza kuwasili leo Ijumaa nchini Afrika Kusini, kwa mkutano wa kwanza ndani ya bara la Afrika, wa kundi la mataifa tajiri na yanayoinukia kiuchumi ya G20.

Afrika Kusini, Johannesburg 2025 | Nembo ya G20-
Viongozi wa Kundi la G20 waanza kuwasili Afrika Kusini huku Marekani ikisusia mkutano huoPicha: Kyodo News/IMAGO

Mkutano huo unaonuiwa kuweka matatizo ya mataifa masikini barani Afrika, katika ajenda kuu ya mazungumzo, umegubikwa na mvutano kati ya mwenyejiAfrika Kusini na Marekani baada ya utawala wa Trump kuususia.

Mkutano huo unaoanza mjini Johannesburg utahudhuriwa na wajumbe 18 wa mataifa tajiri na yanayoinukia kiuchumi ukiondoa Marekani, ambayo imesema ni aibu kwa mkutano huo kufanyika Afrika Kusini. Trump anadai kuwa waafrika kusini weusi waliowengi wanafanya mauaji ya waafrika kusini wazungu waliowachache nchini humo.

Mkutano wa G20 utajadili pamoja na mambo mengine athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa mataifa yanayoendelea, mzigo wa madeni kwa mataifa masikini na ongezeko la pengo kubwa la ukosefu wa usawa duniani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW