1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Viongozi wa kundi la Quad kukutana pembeni mwa mkutano wa G7

19 Mei 2023

Viongozi wa Kundi la Quad linalozijumuisha nchi za Marekani, Japan, Australia na India watakutana siku ya Jumamosi pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa G7 baada ya mkutano wao wa Sydney kufutiliwa mbali.

Mkutano wa QUAD Tokyo, Japan
Viongozi wa mataifa ya kundi la QUAD walipokutana hivi Mei mwaka 2022 nchini JapanPicha: Masanori Genko/The Yomiuri Shimbun/AP/picture alliance

Viongozi hao walitarajiwa kukutana wiki ijayo baada ya mkutano wa G7, lakini mpango huo ukafutwa baada ya rais wa Marekani Joe Biden kusitisha ziara yake ya bara la Asia kufuatia majadiliano ya mzozo wa deni la Marekani yaliyofanyika Washington.

Kulingana na Ikulu ya Marekani, viongozi hao watakaribisha mbinu mpya za ushirikiano wa mataifa hayo ya Quad katika kupata teknolojia ya kidijitali, nyaya za mawasiliano zinazopatikana chini ya bahari na miundombinu.

Kundi hilo linataka kupambana na uchokozi wa China katika eneo la Asia Pasifiki chini ya Rais Xi Jinping, lakini China imeyaelezea makundi hayo kuwa na nia ya kuizingira kijeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW