Viongozi wa kusini mwa Asia wanuwia kuimarisha ushirikiano.
3 Agosti 2008Colombo
Mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa manane ya kusini mwa Asia unafanyika katika mji mkuu wa Sri Lanka-Colombo, ukiwa na lengo la kuimarisha uhusiano wa eneo hilo na usalama wa chakula.
Masuala yanayoyagubika mazungumzo hayo, ni mapigano kati ya majeshi ya Sri Lanka na waasi wa Kitamili na mvutano baina ya India na Pakistan baada ya mripuko wa bomu kwenye ubalozi wa India katika mji mkuu wa Afghanistan -Kabul hivi karibuni.
Mkutano huo wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano katika kanda kusini mwa Asia SAARC, unatarajiwa kumalizika kwa makubaliano juu ya kupambana na ugaidi, ikiwa ni pamoja na njia za kuzuwia fedha zinazodaiwa kutumiwa na magaidi.
Akizungumzia suala hilo katika hotuba yake, rais wa Sri lanka Mahinda Rajapaksa alitoa wito wa kuongezwa maradufu juhudi za kupambana na ugaidi.
O-Ton Rajapaksa
Pia viongozi hao wanazingatia mpango wa kuunda benki ya chakula ya kimkoa, kuwasaidia wakaazi wao wanaoathirika kutokana na kupanda kwa bei.