Viongozi wa Libya wakubaliana kuunda serikali mpya ya umoja
11 Machi 2024Matangazo
Viongozi hao ni rais wa Baraza la Rais (PC) Mohamed Menfi, mkuu wa Baraza Kuu la Serikali (HSC) Mohamed Takala, ambao wote wanaishi Tripoli, na Aguila Saleh, spika wa Baraza la Wawakilishi (HoR) la huko mjini Benghazi.
Katika taarifa ya pamoja, viongozi hao watatu pia wametoa wito kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na jumuiya ya kimataifa kusaidia ufanikishwaji wa mapendekezo yao.
Mchakato wa kisiasa wa kutatua mzozo wa zaidi ya muongo mmoja nchini Libya ulikwama tangu kuporomoka kwa uchaguzi Desemba 2021 huku kukiwa na mizozo kuhusu uhalali wa wagombea wakuu.