SiasaUkraine
Viongozi wa magharibi waikosoa hotuba ya rais Putin
21 Februari 2023Matangazo
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni anayeitembelea Ukraine ameitaja hotuba hiyo ya Putin kuwa "propaganda" huku mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan akisema madai yaliyotolewa na rais Putin kuwa sababu ya Urusi kuingia vitani ni ya "kipuuzi".
Katika hotuba yake mbele ya bunge la taifa rais Putin alisema mataifa ya magharibi ndiyo yaliilazimisha Moscow kuingia vitani baada ya kugeuka kitisho kwa usalama wa Urusi.
Kwa upande wake mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema madai hayo hayana ukweli kwa sababu rais Putin ndiye alianzisha vita ya kutaka kuishikilia mateka Ukraine na bado anaendekeza uhasama.