1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Viongozi wa makundi ya uhalifu Haiti wawekewa vikwazo

9 Desemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kuwaongeza watu wanne wanaotuhumiwa kuwa viongozi wa makundi ya kihalifu nchini Haiti kwenye orodha yake ya vikwazo.

Umoja wa Mataifa limeidhinisha kuwaongeza watu wanne wanaotuhumiwa kuwa viongozi wa makundi ya kihalifu nchini Haiti
Umoja wa Mataifa limeidhinisha kuwaongeza watu wanne wanaotuhumiwa kuwa viongozi wa makundi ya kihalifu nchini Haiti Picha: Yuki Iwamura/AFP/Getty Images

Hatua hiyo iliyosubiriwa kwa hamu inafikiwa wakati taifa hilo likikabiliwa na mzozo mbaya wa kibinaadamu na ongezeko la miito ya kimataifa ya kupeleka wanajeshi wa kulinda amani kuwasaida polisi wa Haiti waliloelemewa na makundi hayo.

Umoja wa Mataifa umewawekea vikwazo Renel Destina anayeaminiwa kuwa kiongozi mkuu wa kundi la Grand Ravine, Vitel'homme Innocent anayeongoza kundi la Kraze Barye, Johnson Andre wa 5 Segond na Wilson Joseph wa kundi la 400 Mawozo.

Baraza hilo tayari lilimuwekea vikwazo kiongozi wa kundi la G9 Alliance Jimmy Cherizier linalopambana na muungano wa G-Pep, ambayo yote yanataka udhibiti wa eneo kubwa la mji mkuu, Port-au-Prince.