1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Viongozi wa mataifa 18 watoa wito kuwachilia mateka Gaza

25 Aprili 2024

Marekani, Uingereza, Ufaransa na zaidi ya nchi kumi na mbili zimetoa wito kupitia taarifa ya pamoja kwa kundi la wanamgambo wa Hamas kuwaachilia mateka wanaowashikilia.

Maandamano ya familia za mateka wanaoshikiliwa na Hamas
Maandamano ya familia za mateka wanaoshikiliwa na HamasPicha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Viongozi hao wametoa wito wa kuachiwa huru mara moja kwa mateka wote wanaowajumuisha raia wa nchi hizo ambao wameshikiliwa katika Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya siku 200.

Viongozi hao pia wamesisitiza kwamba mapendekezo yaliotolewa ya kuachiliwa kwa mateka yatasaidia kusitisha vita mara moja na kwa muda mrefu katika eneo hilo la Gaza, kuongezeka kwa msaada wa kibinadamu unaohitajika na pia kuchangia kumalizika kwa uhasama.

Viongozi hao wameongeza kuwa wanaunga mkono juhudi za upatanishi zinazoendelea kuwaresha nyumbani raia wao.

Israel inakadiria kuwa takriban watu 129 kati ya 250 waliotekwa nyara wakati wa shambulio la Hamas la Oktoba 7 wamesalia Gaza, wakiwemo watu 34 ambao jeshi linasema wamekufa.