1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Viongozi wa mataifa duniani wazungumza na Trump

7 Novemba 2024

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amefanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa ulimwengu katika wakati anaanza maandalizi ya kuchukua hatamu za uongozi ifikapo Januari mwaka unaokuja.

Rais mteule a Marekani, Donald Trump
Rais mteule a Marekani, Donald Trump. Picha: Alex Brandon/AP/picture alliance

Miongoni mwa viongozi waliozungumza kwa njia ya simu na Trump ni pamoja na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambapo wawili hao wamejadili hali kwenye kanda ya Mashariki ya Kati na kile ofisi ya Netanyahu imekitaja kuwa "kitisho cha Iran".

Rais Volodymyr Zelenskyy  wa Ukraine naye amesema amezungumza na Trump na kwamba wamekubaliana kuimarisha mawasiliano ya karibu na ushirikiano.

Utawala mjini Kyiv unasubiri kwa mashaka kusikia hatua ambazo Trump atachukua kutekeleza ahadi yake ya kumaliza vita kati ya Ukraine na Urusi.

Viongozi wengine waliozungumza na Trump, ni Waziri Mkuu wa Uingereza Kier Starmer, yule wa Hungary Voctor Orban, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Mwanamfalme wa Sauid Arabia Mohammed bin Salman.