1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya kukutana kujadili uhamiaji haramu

10 Desemba 2024

Mawaziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi na Ubelgiji watakutana Jumanne mjini London kujadili tatizo la uhamiaji haramu.

Wahamiaji wakiwa kwenye mashua wakielekea Uingereza
Wahamiaji wakiwa kwenye mashua wakielekea UingerezaPicha: Dan Kitwood/Getty Images

Viongozi hao wanatarajia kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya makundi ya uhalifu yanayohusishwa na vitendo vya uhamiaji haramu barani Ulaya. Viongozi hao watajadili pia namna ya kuzidisha juhudi zao ili kuyadhoofisha makundi ya magendo na kuhakikisha wote wanaohusika na shughuli hizo hatari wanafikishwa mahakamani.

Soma pia: Umoja wa Ulaya wajizatiti zaidi juu ya wahamiaji haramu

Wawakilishi wa Tume ya Ulaya na shirika la kulinda mipaka ya Ulaya Frontex na lile la Polisi ya Ulaya Europol watashiriki pia mkutano huo ili kuelezea mpango kabambe wa utekelezaji wa hatua hizo kwa mwaka ujao wa 2025. Tangu kuanza kwa mwaka huu, takriban wahamiaji 34,000 wamewasili Uingereza wakipitia baharini kwa kutumia mashua na karibu watu 70 wameripotiwa kufa maji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW