1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa mataifa manne yenye viwanda vingi bara la Ulaya wakutana London kujadilia hali ya uchumi kwa sasa

29 Januari 2008

LONDON:

Viongozi mashuhuri kutoka bara la Ulaya wanakutana jijini London ,nchini Uingereza kujadili njia za kuunasua uchumi wa dunia unaoyumbayumba kwa sasa.Viongozi wanaokutana ni rais wa Ufaransa Nicolas Sakozy, Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel, waziri mkuu wa Italy Romano Prodi, rais wa tume ya Ulaya Jose Manuel Barosso na mwenyeji Gordon Brown , wa Uingereza.

Viongozi hao wanataka mfumo bora wa kimataifa wa kubadilishana habari ambao utaweza kutumiwa kuepuka migogoro ya kiuchumi ya hapo baadae.Mkutano wa Barosso na wana chama wa Ulaya wa jumuia ya mataifa manane yenye viwanda umekuja kabla ya mazungumzo ya mawaziri wa fedha wa mataifa ya G7 uliopangwa kufanyika Febuari 9 mjini Tokyo nchini Japan.