1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa NATO wakutana Washington chini ya wingu la vita

9 Julai 2024

Viongozi wa nchi za Jumuiya ya kujihami ya NATO wanakutana kwa lengo la kuiunga mkono Ukraine dhidi ya Urusi,ingawa mkutano huo unatarajiwa kugubikwa na suala la rais Joe Biden kupambania uhai wake wa kisiasa.

Zelenskyj anakutana na uongozi wa Poland huko Warsaw
Rais Volodymyr Zelensky Kabla ya mkutano wa kilele wa NATO mjini Washington, pale alipokutana na uongozi wa Poland mjini Warsaw.Picha: Radek Pietruszka/PAP/dpa/picture alliance

Kiongozi huyo wa Marekani anatarajiwa kutumia mkutano huo wa siku tatu wa maadhimisho ya miaka 75 tangu ulipoanzishwa mfungamano huo wa kiulinzi,kuwahakikishia washirika wake juu ya uongozi wa Marekani na uwezo wake wa kuliongoza taifa hilo, wakati miito ikiongezeka ya kumtaka ajiondowe kwenye kinya'ng'anyiro cha kuwania muhula wa pili madarakani. Hata hivyo viongozi wa NATO wanatarajiwa kuonesha bado wanatambuwa hali halisi inayoendelea katika uwanjawa vita nchini Ukraine. Rais Volodymyr Zelensky nae pia atashiriki mkutano huo wa Washington akiwa na matumani ya kupata msaada wa mifumo zaidi ya ulinzi wa anga aina ya Patriot ambayo,kwa miezi kadhaa amekuwa akiiomba kwa washirika wake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW