1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya kukutana kwa mazungumzo juu ya Ukraine

13 Machi 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anajiandaa kukutana na rais Emmanuel Macron pamoja na waziri mkuu wa Poland, Donald Tusk mjini Berlin, juu ya sera kuhusu Ukraine.

Hamburg | Emmanuel Macron na Olaf Scholz
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: IMAGO

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anajiandaa kukutana na rais Emmanuel Macron pamoja na waziri mkuu wa Poland, Donald Tusk mjini Berlin,Ijumaa katika wakati ambapo tofauti zimeongezeka kati ya Ufaransa na Ujerumani juu ya sera kuhusu Ukraine.

Taarifa hiyo imechapishwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Politico leo na kuthibitishwa  pia kwa shirika la habari la kijerumani,dpa na vyanzo vya serikali.Mkutano huo ni wa kwanza wa viongozi wa juu wa kile kinachojulikana kama, Weimar Triangle yaani muungano wa kikanda wa pande tatu, tangu Juni mwaka jana.

Soma: Ukraine yaihimiza Ujerumani kuipatia makombora ya Taurus

Mkutano huo utakaofanyika Berlin, unakuja wiki tatu baada ya viongozi wa serikali wa nchi 20 kukutana Paris nchini Ufaransa na kujadili mgogoro wa Ukraine,ambapo ulimalizika kwa kuibuka mivutano na kutokubaliana kuhusu uwezekano wa kupeleka wanajeshi nchini Ukraine.