1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Sudan waahirisha kutiwa saini makubaliano

1 Aprili 2023

Viongozi wa Sudan wameahirisha kutiwa saini kwa makubaliano kulikopangwa kufanyika Jumamosi ili kurejesha kipindi cha mpito cha demokrasia, huku hali ya kutoelewana baina ya makundi ya kijeshi ikiendelea.

Sudan |  Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan
Picha: Mahmoud Hjaj /AA/picture alliance

Viongozi wa Sudan wameahirisha kutiwa saini kwa makubaliano kulikopangwa kufanyika Jumamosi ili kurejesha kipindi cha mpito cha demokrasia, huku hali ya kutoelewana baina ya makundi ya kijeshi ikiendelea.

Mapinduzi ya Oktoba mwaka 2021 yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhanyalivuruga mchakato ulioanza, kufuatia kuondolewa madarakani kwa Omar al-Bashir mwaka 2019.

Khaled Omar Youssef, aliyeondolewa madarakani na kukamatwa wakati wa mapinduzi ya Burhan na ambaye sasa ndiye msemaji wa mazungumzo hayo, amesema kwamba mkutano mpya kati ya makundi ya kijeshi na ya kiraia umepangwa kufanyika baadaye leo Jumamosi.

Kwa wiki kadhaa, wawakilishi kutoka pande zote wamekuwa wakijadiliana sehemu ya mwisho katika mchakato wa kisiasa uliokuwa na awamu mbili na kuzinduliwa mwezi Disemba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW