1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ujerumani wajumuika kwa miaka 33 ya muungano

4 Oktoba 2023

Viongozi wa Ujerumani wametoa wito kwa umma wa taifa lao kuungana wakati taifa hilo likiadhimisha miaka 33 tangu muuungano wa iliyokuwa Ujerumani mashariki na Ujerumani magharibi.

Deutschland | Tag der Deutschen Einheit in Hamburg | Elbphilharmonie
Picha: Gregor Fischer/Pool AP/dpa/picture alliance

Tarehe rasmi ya muungano huo ni Jana, Oktoba 3.

Katika maadhimisho hayo kitaifa ambayo yamefanyika mjini Hamburg, meya wa jiji hilo, Peter Tschentscher amewaomba Wajerumani kuonesha uzalendo katika kipindi hiki cha changamoto kadhaa akisema ni Ujerumani yenye nguvu ya kidemokrasia inaweza kuwa na wajibu kwa Ulaya madhubuti ambayo inajitolea kwa amani, demokrasia na haki za binadamu.

Kansela Olaf Scholz and Rais Frank-Walter Steinmeier walikuwa miongoni mwa wageni 1,300 ambao walihudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika jengo maarufu la Hamburg, Elbphilharmonie.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW