1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya hawana wasi wasi na kura ya Cyprus

20 Machi 2013

Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades anakutana na viongozi wa vyama vya kisiasa katika hatua ya dharura ya kutafuta mpango mbadala baada ya bunge kukataa mpango wa Umoja wa Ulaya wa uokozi.

GettyImages 164064657 Cypriot members of parliament (MPs) vote on a controversial bailout agreement with a troika of international lenders during a parliament session in the capital, Nicosia, on March 19, 2013. Cyprus MPs overwhelmingly rejected a tax on bank deposits demanded by international lenders as a condition for a bailout deal, with a vote of 36 against, 19 abstentions and none in favour. AFP PHOTO/YIANNIS KOURTOGLOU (Photo credit should read Yiannis Kourtoglou/AFP/Getty Images)
Wabunge wa Cyprus wakipiga kuraPicha: AFP/Freier Fotograf

Kundi la mataifa yanayotumia sarafu ya euro limeelezea kwa tahadhari matokeo ya kura bungeni nchini Cyprus. Wakati huo huo lakini viongozi wa juu wa umoja wa Ulaya wanazungumzia zaidi kuhusu yaliyotokea nchini Cyprus.

Mkutano wa dharura katika ikulu ya rais nchini Cyprus pia unahudhuriwa na gavana wa benki kuu Panicos Demetriades na wajumbe wa kundi la pande tatu la wafadhili , Umoja wa Ulaya , benki kuu ya Ulaya na shirika la fedha la kimataifa IMF.

Rais Nikos AnastasiadesPicha: picture-alliance/dpa

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameeleza nia yao ya kuendelea kuisaidia Cyprus licha ya bunge la nchi hiyo kukataa masharti ya umoja huo. Waziri wa fedha wa Uholanzi Jeroen Dijsselbloem amesema ameyakubali matokeo ya bunge la Cyprus.

"Ni kweli kwamba inakatisha tamaa. Nasikitika kuwa Cyprus imefikia uamuzi huu. Lakini mpira bado uko upande wao , pendekezo la mpango wa uokozi la mataifa ya euro linaendelea".

Maandamano ya kupinga wateja kukatwa fedha zaoPicha: picture-alliance/dpa

Waziri wa Ujerumani aonya

Waziri wa fedha wa Ujerumani lakini ameonya kuwa , Wacyprus wasitarajie kupata matumaini ambayo hayawezekani.

"Matumaini ya Wacyprus hayawezi kuendelea kama yalivyo na kujaribu kuvutia mitaji, ambayo haijawekezwa na inagharamiwa na watu wengine, kwa kuwa utaratibu huo hauwezi kufanyakazi, hii ni hali ya kufikirika tu. Na viongozi nchini Cyprus ni lazima wafafanue kwa watu wao".

Cyprus yatoza kodi fedha za wateja

Chini ya masharti ya kupatiwa mpango huo wa uokozi uliofikiwa mwishoni mwa juma, kundi la pande tatu lilitarajiwa kuipatia Cyprus kiasi cha euro bilioni 10 kwa masharti kuwa nchi hiyo itafute yenyewe kiasi cha euro bilioni 5.8.

Nchi hiyo iliweka kodi ya asilimia 9.9 kwa fedha za wateja zilizoko katika benki nchini humo, na hatua hiyo ilizusha hasira miongoni mwa watu walioweka fedha zao na kuleta hofu kuwa mataifa mengine ya umoja wa Ulaya yenye matatizo ya kifedha kama Italia, na Uhispania huenda yakafuata mkondo huo.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang SchäublePicha: picture-alliance/dpa

Serikali ya Cyprus ilibadilisha msimamo, na jana Jumanne iliachana na pendekezo la kutoza kodi hiyo kwa fedha chini ya euro 20,000 , wakati ikiendelea na mpango wake wa kutoza asilimia 6.75 kwa fedha zilizowekwa kuanzia euro 20,000 hadi 100,000 na asilimia 9.9 kwa fedha zinazovuka kiwango hicho.

Lakini hatua hiyo pia ililalamikiwa na spika wa bunge la nchi hiyo na kusema ni kama uporaji.

Mwandishi : Andreas Reuter / ZR / Kitojo Sekione

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW