Viongozi wa EU wakutana Budapest kufuatia ushindi wa Trump
7 Novemba 2024Viongozi wa Umoja wa Ulaya leo wamejaribu kuonyesha msimamo wa katikati wakisisitiza umuhimu wa kujitegemea katika masuala ya usalama ila wakati huo huo wakizungumzia umuhimu wa ushirikiano wa kiuchumi na Marekani.
Hii ikiwa ni siku moja tu baada ya Donald Trump kushinda muhula wa pilikatika uchaguzi wa Marekani. Rais wa Hamashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyene amesema Umoja wa Ulaa ni sharti "kusalia katika mkondo wake" iepuke changamoto zake na ijitegemee kiusalama na kiuchumi.
Viongozi hao wa Ulaya wanakutana huko Budapest ambapo ajenda za mkutano wao zilikuwa ni uchumi, uhamiaji, uchaguzi wa hivi majuzi georgia, mzozo unaotanuka wa Mashariki ya Kati na uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine.
Ila kurudi madarakani kwa Trump kumepelekea ajenda kubadilika huku viongozi wa Ulaya hasa katika Umoja wa Ulaya na nchi zinazopakana na Urusi, zikiwa zinapitia kipindi kigumu kuyakubali matokeo hayo ya uchaguzi wa Marekani na maana yake kwa mahusiano yao na Marekani.