1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya wakutana Granada katikati mwa mizozo

5 Oktoba 2023

Katika mkutano wa tatu wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya, EPEC, mjini Granada, mizozo inayoongezeka na mivutano katika bara hilo vitakuwa juu kwenye ajenda. RAsmi, viongozi hao watajadili usafiri, nishati na akili bandia

Gipfeltreffen der Europäischen Politischen Gemeinschaft l Kanzler Scholz am BER Flughafen, Berlin
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na wenzake walitarajiwa pia kuibua masuala yakiwemo athari za teknolojia bandia pamoja na usalama wa nishati na uhamaji kuelekea nishati jadidifu kwenye mkutano EPC.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Rasmi, viongozi wanaokutana katika jiji la Uhispania la Granada kwa mkutano wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya (EPC) watajadili usafiri, nishati na akili bandia.

Mada hizo ziko kwenye ajenda rasmi ya mkutano huo, lakini mkutano wa viongozi 47 wa Ulaya pia utashughulikia masuala kama vile vita vinavyoendelea vya Urusi nchini Ukraine, uhamiaji na kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi za EPC kama vile Armenia na Azerbaijan na kati ya Kosovo na Serbia.

Wazo la EPC, ambalo lilianzishwa tu mwaka jana, ni kwamba inapaswa kusaidia nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuwasiliana vyema na nchi za Ulaya ambazo si sehemu ya umoja huo. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anahudhuria mkutano huo mjini Granada. Vita vya Urusi nchini Ukraine huenda vikatawala tena mkutano huo.

Viongozi wa Ulaya walitarajiwa kumhakikishia Zelenskyy msaada wa muda mrefu, ishara muhimu baada ya msaada zaidi wa kijeshi kwa Kyiv kutojumlishwa katika mpango wa bajeti ya bunge la Marekani mwishoni mwa juma.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy anahudhuria mkutano wa EPC.Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Zelenskyy aliandika kwenye mtandao wa X, zamani Twitter, kwamba alitaka kutoa kipaumbele maalum "kwa eneo la Bahari Nyeusi pamoja na juhudi zetu za pamoja za kuimarisha usalama wa chakula duniani na uhuru wa usafiri wa baharini."

Mazungumzo ya Azerbaijan na Armenia kwenye mkutano wa kilele

Mkutano kati ya viongozi wa Azerbaijan na Armenia, wa kwanza tangu operesheni ya kijeshi ya Baku kuchukua udhibiti wa Nagorno-Karabakh mwezi uliopita, ulifutwa. Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev aliamua kutohudhuria mkutano huo.

Soma pia: Mkutano wa viongozi wa mataifa ya Ulaya mjini Prague kutuma ishara wazi kwa Urusi

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuzuia kuongezeka zaidi kwa mzozo, lakini Aliyev amekasirishwa na "taarifa zinazounga mkono Armenia kutoka kwa maafisa wa Ufaransa" na kwa sababu Paris imesema inapanga kuipelekea Yerevan vifaa vya kijeshi, afisa wa Azerbaijan alisema.

Afisa huyo alisema uamuzi wa Aliyev pia ulihusu matamshi ya Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel. Michel, ambaye amekuwa mpatanishi wa mikutano kadhaa kati ya mahasimu hao wawili katika miaka ya hivi karibuni, alikosoa matumizi ya nguvu ya kijeshi ya Baku.

Sunak na Meloni kushinikiza hatua kali juu ya uhamiaji

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na mwenzake wa Italia Giorgia Meloni watakutana na washirika wengine wa Ulaya kando ya EPC kujadili "hatua ya pamoja" dhidi ya "uhalifu uliopangwa wa wahamiaji."

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Suna, akifurahia jambo na mwenzake wa Italia, Georgia Meloni.Picha: Ludovic Marin/Reuters

"Viwango vya uhamiaji haramu kuelekea bara la Ulaya ni vimekuwa vya juu zaidi katika takriban muongo mmoja. Huku maelfu ya watu wakifa baharini, wakipelekwa na walanguzi wa watu, hali ni ya ukosefu wa maadili na si endelevu," Sunak alisema katika taarifa yake kabla ya mkutano huo.

Soma pia: Je Umoja wa Ulaya na washirika wake wanaweza kuleta utulivu Libya?

"Hatuwezi kuruhusu magenge ya wahalifu kuamua ni nani anayekuja katika ufuo wa Ulaya."

Mkutano wao unakuja licha ya makubaliano ya mafanikio ya wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya mwanzoni mwa juma juu ya mpango wa mageuzi ya uhamiaji kwenda mbele ya Bunge la Ulaya kugawana vyema jukumu la wanaowasili wasio nyaraka.

Mkutano wa Alhamisi wa EPC utafuatiwa siku ya Ijumaa na mkutano wa viongozi 27 wa EU, huku mazungumzo yakitarajiwa kulenga upanuzi na uhamiaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW