Viongozi wa Ulaya wazungumzia ukosefu wa ajira
12 Novemba 2013Viongozi hao wanakutana kwa mara nyingine wakati ambapo idadi ya vijana wasiokuwa na kazi inaongezeka barani Ulaya. Hivi karibuni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitoa mwito wa kufanya juhudi thabiti ili kulishushuhgilkia tatizo la ukosfu wa ajira miongoni mwa vijana barani Ulaya.
Kwenye mkutano wao wa kilele wa hivi karibuni viongozi wa Umoja wa Ulaya waliazimia ,kuhakikisha kwamba hakuna kijana mwenye umri wa chini ya miaka 25 atakaepaswa kusubiri kwa muda wa zaidi ya miezi minne ili kupata kazi au nafasi ya kujifunza kazi.Jee azimio hilo limeleta nini kwa vijana wa Ulaya? Mwaka uliopita Halmashauri ya Umoja wa Ulaya ilipendekeza mpango wa hatua kadhaa wenye lengo la kuzuia ongezeko la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.
Pamoja na hatua hizo ni kutenga kiasi cha Euro Bilioni nane kwa ajili ya kupambana na ukosefu wa ajira. Bilioni nyingine moja imeongzwa na Halmashauri ya Umoja wa Ulaya kwa kupitia kwa nchi wanachama na kwa kupitia kwa mfuko wa kijamii wa Ulaya.
Hata hivyo katika juhudi za kukabiliana na mgogoro wamadenei nchi za Ulaya zimepitisha sera zinazokingamana na juhudi za kupambana na ukosefu wa ajira. Mbunge wa chama cha social demokratik kwenye bunge la Ulaya Jutta Steinruck ameitaka serikali yakila nchi ya Umoja wa Ulaya iweke mazingira yatakayowezesha kutengwa kwa nafasi za kazi. Tunahitaji miundo itakayowezesha kutengwa kwanafasi za ajira za muda mrefu. Na kwa ajili hiyo serikali zitapaswa ziweke fedha tayari ili kuwezesha kutenga nafasi za kazi zitakokuwa bora"
Mbunge huyo Jutta Steinruck amezikosoa sera za Umoja wa Ulaya, Shirika la fedha la kimataifa,IMF na za Benki Kuu ya Ulaya , ECB zinazoelekezwa katika kubana matumizi. Amesema sera hizo zimetekekeza nafasia za ajira.
Mbunge huyo pia amesema sera hizo zimesababisha nchi kuzama zaidi katika mdororo wa uchumi. Nchi ambazo hasa zimekumbwa na mgogoro wa madeni ni Uhispania,Ugiriki na Ureno. Wachunguzi wanasema kutokana ma bajeti za nchi kuwa ngumu, viongozi wanaokutana leo mjini Paris hawatarajiwi kupiga hatua ndefu zaidi katika juhudi za kulitaua tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana. Asilimia 23.5 ya vijana barani Ulaya kwa sasa hawana kazi.
Mwandishi: Pabst,Sabrina.
Tafsiri; Mttullya Abdu.
Mhariri: Josephat Charo