1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUhispania

Wakuu wa Umoja wa Ulaya wakutana Granada

6 Oktoba 2023

Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Granada Uhispania kujadili baadhi ya matatizo makuu yanayoukabili umoja huo ikiwemo uhamiaji na siasa za kikanda.

Baadhi ya wakuu ya Ulaya wakiwa katika mazungumzo kabla ya mkutano baina yao unaofanyika Granada nchini Uhispania, Oktoba 5, 2023
Baadhi ya wakuu ya Ulaya wakiwa katika mazungumzo kabla ya mkutano baina yao unaofanyika Granada nchini Uhispania, Oktoba 5, 2023Picha: Ludovic Marin/AFP

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni anatarajiwa kuzungumza na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz pembezoni mwa mkutano huo wa kilele, baada ya Meloni kushangazwa na msaada wa kifedha wa Ujerumani kwa mashirika ya uokoaji wa wahamiaji wanaojikuta hatarini baharini Mediterania.

Aidha wanatarajiwa kujadili vipaumbele vya kimkakati vya umoja huo katika miaka ijayo, ikiwemo uwezo wa kiulinzi, upatikanaji wa nishati, majibu ya pamoja dhidi ya mizozo ya hali ya hewa na uchumi wa umoja huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW